lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu roma mkatoliki – mkombozi feat one six

Loading...

owoo, owoooo
aaah aah…
aaah bado napolia mama
eh eh eh eeeh eeeeh

(tongwe records)
bin laden

napiga goti napiga ishara ya msalaba
dunia imenipiga kofi namuomba baba la baba
nipimie shoti ya bapa nizime mada
asubuhi nigongee noti niende kuifanya ibada
nadaiwa kodi ya pango, nadaiwa ada ya watoto
na mama wa kambo anamchuna baba
na baba yuko ng’ambo ni mwaka sijaona msaada
ama kweli dunia ina mambo hadi jogoo anaweza taga
jirani ananiambia be humble, be humble
nikipiga kizinga we unafunga mlango
that’s ridiculous (hahaha) it’s now funny am serious
am g~nius, though inanitesa am notorious
baba hakutupa urithi, wa pasi wala feni
wala peni ambayo ingenipa elimu shuleni
bali alituachia madeni na sifa mbaya ukweni
sa huyo ndo baba gani? humble au mtemi?

na mtaani kuna binti nimempa mimba
mtoto wa mjeda muda wote pira litatimba
na sina dusko so kwa doctor siwezi timba siwezi vimba
na kila chocho bongo wananiwinda

nimekesha kwa waganga
nimevunja n~z~ njia panda
nimeshikishwa tunguli msata
mkata nikambeba manyanga
mikesha ya kinabiii
nyumba zote za ibada
nimeshiriki sana
m~n~sura kukufuru sijaumbwa na wewe

k~mbe yupo mungu, mkombozi
wa kukufuta machozi
pale unapolia mwana
we baba (yeiii wowowowo)
k~mbe yupo mungu, mkombozi
wa kukufuta machozi
pale unapolia mwana
we baba (yeiii wowowowo)

nishaiba nikaenda mabusu na ndugu hawakuja niona
na wakasema hayawahusu mwizi anatakiwa kuchomwa
nilipotoka nikawabusu wakasema nimewasonya
nikaona eeh maji mazito kuliko damu ya roma
ukiendekeza ndugu, utavuna magugu
utakufa kibudu na mungu hutamwabudu
utamkataa wa joto utamkana wa baridi
atabakia wa vuguvugu naye pia ataleta gubu
usi~complicate, stress inaleta frustration
be patient, anguko kubwa ni kuikosa attention
its not fair, nawapa proposal they don’t care
na watasema huna demand fitina watakuekea
huku nadaiwa vikoba, kule nadaiwa rejesho
naenda kujificha goba, usiku narudi keko
nawaza hata kuroga nikiamini nitaipata kesho
au nisali sala ya toba nijiue nikwepe mateso
ooh jesus, fanya miujiza
naona giza ukija mw~nga unaniumiza
so please kama unaniskiza naijongea altare
useme neno moja tu naahidi nitakesha pale

nimekesha kwa waganga
nimevunja n~z~ njia panda
nimeshikishwa tunguli msata
mkata nikambeba manyanga
mikesha ya kinabiii
nyumba zote za ibada
nimeshiriki sana
m~n~sura kukufuru sijaumbwa na wewe
k~mbe yupo mungu, mkombozi
wa kukufuta machozi
pale unapolia mwana
we baba(yeiii wowowowo)
k~mbe yupo mungu, mkombozi
wa kukufuta machozi
pale unapolia mwana
we baba(yeiii wowowowo)

we baba, we mwana
aah pale unapolia mama
(eh eh eeh eeeh)

k~mbe yupo mungu, mkombozi
pale unapolia mama
we baba eeeh eeh

k~mbe yupo mungu, mkombozi
pale unapolia mama
we baba eeeh eeh

(tongwe records)
bin laden


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...