lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu nikki mbishi – utamaduni

Loading...

verse i:
yo, vina punch na midundo, mafumbo na temithali
za semi, zisome tungo, ni gumzo, jiweke mbali
mi ni fundo we ni mwali nishike udumishe ndoa
bila mishe niko poa nipishe nisafishe doa
nadharia kwa kilinge, ninge hazitambi tena
nishinde mbilinge, mungu hazijui dhambi njema
gongo la mboto msoto hainyweki gongo ya moto
maisha vitisho, mwisho wanaujua hadi mrisho mpoto
kafara za kuchinja fake wanachimba
kila napo timba wanapotea ki mazingara kama ninja
choir master bubu, rasta choma kaya, fire
si husudu mabaya, hii ni saa mbaya, muhaya tubu
napanga mistari mithili watoto wa kaya za kipemba
mashairi ka riwaya za andanenga
nafunza kwa kilingi
kama tenzi ni hela ubongo w-ngu ni benki, so n-z-tunza ka shilingi
blow kiss kama jada, makada ndio sisi
we radar police, snitch vipi unidiss bila mada?
wonder kama stevie na hii flow ndiyo yenye mwali
inayokubamba kama mwizi na siku hizi emcees hawalali

hook:
ni utamaduni, au sio, sio mbio za sakafuni
j-po umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio
shika kanuni za majilio
nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio
au sio, sio mbio za sakafuni
j-po umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio
shika kanuni za majilio
nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio

verse ii:
bashiri unavyoweza, au beza inapostahili
au tabiri kama pweza, jeneza linamsubiri
na eneza mashairi mithili ya injili ya ebeneza
kiswahili, kiingereza nacheza mahiri naweza
nawapa somo wana, bila kikomo nachana
media zinabana promo, na mdomo bado umeachama
katuni tupa kapuni, na kupa kanuni
supa kapuka hazivumi, shtuka, zinduka na utamaduni
mbishi ni oversize, nivae nikuvuke
we ni mayonnaise kwenye mkate, ngoja uchakae baadae wakutupe
ndani ya kilinge nitinge, chui ni vimbe
we hujui mbinde, msondo huijui ngoma ya sikinde
na survive na vibe za live bendi
mi na mengi ya ku-describe, sio pride ya ku-drive range
hii ni wazi, nina hadhi ya wako role model
na sio stori ndogo, ka una maradhi twende loliondo
we ni james bond toy, mi ni james bond mtu
wanarespond, lecture ka za desmond tutu
siyo choo cha kike, hiki ni choo cha mashoga
sina uoga napo flow, na hii siyo show ya mapouka

hook:
ni utamaduni, au sio, sio mbio za sakafuni
j-po umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio
shika kanuni za majilio
nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio
au sio, sio mbio za sakafuni
j-po umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio
shika kanuni za majilio
nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio

verse iii:
hakuna dili itafanyika, bila kuweka pesa mob
nipe job ya uhakika, ni show ka nesta bob
na rob akili zenu kwa rhymes, beat na flow
unadata kisha unafyata ile time sh-t inablow
9-1-1 danger, emergency call
mbona game imejaa ma-stranger, hii siyo basketball
uwe tall, alafu unamudu ma-slum dunkin’
au elvis presley, king wa jam funky
mi ndio actor, wa movie isiyo na scripty
macho kwenye paper, michuzi uzi kwa snitchy
mistari mijeledi inachapa kisha inachana
akili ingekuwa nywele wenye dread w-ngeshindikana
na design mbinu za kuwaibia, ka fundi frank
pesa taslimu, haina cha skonyo za hundi benki
bongo bwana, huwezi kukuta magaidi jela
bali wezi wa kuku ka chege wa saidi fella
swing dozen, chini nna buti kali
bitozi na mapozi, mitaani hutafuti ugali
mida mibovu, so mbishi nna skuti mbali
street hukuti mwali, bali ni species za __

hook:
ni utamaduni, au sio, sio mbio za sakafuni
j-po umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio
shika kanuni za majilio
nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio
au sio, sio mbio za sakafuni
j-po umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio
shika kanuni za majilio
nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...