lirik lagu eric wainaina – daima
[mstari 1]
umoja ni fahari yetu
undugu ndio nguvu
chuki na ukabila
hatutaki hata kamwe
lazima tuungane, tuijenge nchi yetu
pasiwe hata mmoja
anaetenganisha
[chorus]
naishi, natumaini
najitolea daima kenya
hakika ya bendera
ni uthabiti w-ngu
nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
daima mimi mkenya
mwananchi mzalendo
[mstari 2]
kwa uchungu na mateso
kwa vilio na uzuni
tulinyakuliwa uhuru
na mashujaa wa zamani
hawakushtushwa na risasi
au kufungwa gerezani
nia yao ukombozi kuvunja pingu za ukoloni
[chorus]
naishi, natumaini
najitolea daima kenya
hakika ya bendera
ni uthabiti w-ngu
nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
daima mimi mkenya
mwananchi mzalendo
[daraja]
wajibu wetu
ni kuishi kwa upendo
kutoka ziwa mpaka pwani
kaskazini na kusini
[solo]
[chorus]
naishi, natumaini
najitolea daima kenya
hakika ya bendera
ni uthabiti w-ngu
nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
daima mimi mkenya
mwananchi mzalendo
[mwisho]
kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
daima mimi mkenya
mwananchi mzalendo
Lirik lagu lainnya:
- lirik lagu vials – iykyk
- lirik lagu mardy price – no feelings
- lirik lagu t.latt – timothy
- lirik lagu howlin’ circus – your light keeps on
- lirik lagu donatella rettore – presto ch’è tardi
- lirik lagu chevralet ss – bad mother-fucker (bmf)
- lirik lagu jennifer rostock – der kapitän
- lirik lagu la arrolladora banda el limón – asi fue
- lirik lagu j.o the corrupted – follow the plan
- lirik lagu terry scott taylor – when the sun comes out again (acoustic demo)