lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu dizasta vina – tatoo ya asili

Loading...

amezongwa na zimwi
alisikia jirani akitoa hoja kwa kijiji
sababu ya kukosa elimu ya maambukizi
walihisi kurogwa ndio sababu ya gonjwa la ukimwi

huyo ni mgonjwa jamani
kama wagonjwa wengine alisema mwalimu
mwenyekiti alimwambia kaa kimya
sio unaropoka kama mwendawazimu

elimu ya mwalimu ilikuwa nuru potevu
nuru ambayo haifiki gizani
ikawekwa idhini mezani kuuwa mizimu imechukia
mgonjwa af~kuzwe kijiji cha mbali

akasindikizwa njiapanda
mwisho wa kijiji mwanzo wa msitu mkubwa wa sanza
alitengwa kama walivyotengwa wengi
kwa mila na desturi zilizoanza tangu enzi

kibuyu cha maji furushi la matunda
na makubazi yaliyoalika funza
hakuna hodi inapofika kiama
mama na nyika nyika na mama

na alikuwa peke yake na ule mzigo mdogo mgongoni
wasiwasi usoni mtoto tumboni
alitamani matawi yaanguke yamtunze
dhidi ya baridi ya mji uliosahaulika na wabunge
umauti aliuhisi
alijitazama na hakuona tofauti na maiti
alilia peke yake porini huku sauti yake
ikisindikizwa na sauti za fisi

wadudu wenye sumu nyingi walimvizia
alikutana na visiki alipotaka njia
mvua kubwa ilinyesha kuonyesha
hata hali ya hewa ilimsaliti pia

alivuka salama mpaka ng’ambo
akajikongoja mpaka kando
kando kwenye mti mkubwa uchungu ulimshika
alizaliwa mtoto mdogo huku mama anakufa

ujinga uliotamalaki kwa kijiji
ndio ujinga uliomnyima haki ya kuishi
alipambana mpaka ilifika tamati pumzi
akamwacha mwanae na zawadi ya virusi

natoa nukuu kariri
mtoto alifunikwa na nguo kuu kuu kwenye mwili
alikuwa na madoa makuu mawili
katikati ya mgongo mfano wa tatuu ya asili

ninatokwa na mate
alisikika kijana akitoa hoja kwa wenzake
waliopanga foleni kwenye chumba chenye mw~nga
hafifu kila mmoja akiingoja zamu yake
walikuwa vijana sita wenye umri wa shule
usipojua thamani utahisi wanaivuta pumzi ya bure
alilala msichana kati ya hawa
kwenye matandiko machafu yalioarika chawa

jamani huyu ni mtoto bado
alisikika mmoja aliyeegemea ndoo ndogo kando
walimfokea alipokataa kushiriki tukio
wakimfananisha na mbwa asiyevuka uzio

walimvua msichana nguo zake za mwili
walimpiga alipojaribu kuficha sehemu zake za siri
alibakwa kama walivyobakwa wengi
kwa tabia za vijana zilizoanza tangu enzi

hawakujua kuhusu mpaka wa hamu
halali na haramu kila mmoja alimbaka kwa zamu
alitendewa uasi
kwa vijana walioshindwa kulelewa na wazazi

mfano wa mlo wa hija walimfakamia
aliliona giza alipotaka njia
alisema imetosha ila hakuna aliyemsikia
maana wengine dada zao walibakwa pia

alitakiwa awe nyumbani labda
kalala kak~mbatia mwanasesere kitandani labda
alilia na sauti yake haikukidhi
kwa sababu hata mji ulisahaulika na polisi
msimuliaji toka chini nalia juu
nasimulia yaliyotukia huruma inaniingia
lakini sina cha kufanya kwa sababu
kazi yangu mi’ kusimulia tu

kuta zingeongea zingeusema huu ukatili
wa maumivu ya juu ya mwili
kuta zingesema alikuwa na madoa makuu mawili
kati’ ya mgongo mfano wa tatuu ya asili


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...