lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu dizasta vina – mlemavu

Loading...

yeah!! haujui wimbo ulio bora dhahiri
haujui ushairi au mstari ukaukariri
haujui giza haujui baridi
au mbu walonighasi wakati nakusubiri

haujui kupenda, moyo wako hewa
wote tumejifunza ila mwenzangu umechelewa
kaa kimya hauna hata haki ya kusema
upuuzi unaofanya sio ushujaa ni ukilema

natamani upate ki~mista pengine
kikuumize kama ulivo’waumiza wengine
unaumwa mama hata kwa matibabu hautopona
sio dhahabu naijua dhahabu nikiiona
kuvimba kwako kamwe hakutavunja miamba
ipo siku utajua kuwa kuringa si afya
utatafuta upendo na utazikuta siasa
utaelewa inavyouma pindi unapofanywa wa ziada

kutojibu jumbe za simu sijui ndio kula njama
kudanganya mahali ulipo umeshavuka zama
huu ushenzi ni uzamani upo nyuma mama
unapodhani ni ujanja nakuonea huruma sana

eti queen, queen hawezi choropoa mimba
ungekufa kwa ngoma kinachokuokoa kinga
unajirusha sana itakukatikia kamba
utazubaa na uzee utakukutia njiapanda

unanuka sana unanitia kichefuchefu
nimepoteza muda umenirudisha nyuma stepu
tunda huishia tumboni likianzia kwenye mbegu
mama nimeshindwa sasa nawaachia walimwengu

nakupigia simu hupokei, nakutext ku~reply una~vex (vex)
kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi hivyo unajiona keki, mlemavu
kutokujua kupenda si ujanja ni ulemavu (yay yay yay yah)

kwenye simu ulivyoni~save mi’ fundi bomba
ndo’ nikajua inavyokata stimu kujikosha
mioyo uliyoichukua ukaichezea na kuitupa
utaenda mbali siku utarudi kuitafuta
na hautaiona tena, aisee utaweweseka
utapojua uzuri hauzuii kuzeeka
utakufa hautaacha alama wala ngao
kama urithi zaidi ya picha chafu kwenye mitandao

namwonea huruma bwana’ko wa sasa si uongo
huko aliko anahisi ameliokota dodo
k~mbe chizi uliyeshindikana milembe
na kama unajiona mzuri sana jipende

mchoyo mama una mtima wa aina gani
utaacha lini hizo bima za wahisani
moyo wako haujui kupenda asirani
haujawahi hata kulala na picha kitandani

haujawahi kuona watu wakighairi masomo
wan~z~jua sheria, lakini bado wanavunja sababu ya kupenda
wanakaidi maonyo
haujui chochote zaidi ya hizo style za ngono

rafiki yako mage tumetoka k~mzika
wenye akili tumejifunza kwa huu msiba
lakini wasio na haya, hawajui kuwa hakuna tuzo ya umalaya
mwanaizaya pumzika

ulinibeba ili uje kunitupa
nilijiachia nimeumia sa’ nimejifunza
siwezi ‘sema hautapata bwana kama mimi
tupo wengi lakini utanik~mbuka naamini
nakupigia simu hupokei, nakutext ku~reply una~vex (vex)
kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi hivyo unajiona keki, mlemavu
kutokujua kupenda si ujanja ni ulemavu (yay yay yay yah)

nakupigia simu hupokei, nakutext ku~reply una~vex (vex)
kwakuwa we ni mzuri unatafutwa na wengi hivyo unajiona keki, mlemavu
kutokujua kupenda si ujanja ni ulemavu (yay yay yay yah)


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...