lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu dizasta vina – hatia ii

Loading...

ah!
nilipaa sasa natua
kwenye/kwenye
siri ya moyo
na siri ya moyo
anayeijua mwenye/
mwenye ujasiri wa
kutunza nafanya
ninachodhani ni
sahihi kitachotokea
nitajua mbele

wanasema mwanaharamu
haijui laana/ kashalaanika
nasikitika kuwa haujui
kama/ naonekana ka’
kondoo kwa mchungaji
lakini…lakini kwa ndani
mi’ ni chui mama

kwa mfano nakuita mpenzi/
na tabasamu zuri wakati
najua kuwa sikupendi/
kuitoa hii siri ndo’ siwezi/
kwahiyo nitakudanganya
mpaka ifike siku niutimize
ushenzi

huwa nawaza nikuweke
ufahamu/ mtambue
kuwa mpo wengi
na lengo niwateke
kwa zamu/ niwaumize
ili mpeleke salamu/
masikini mrembo
nashangaa jinsi unavo’ngoja
pete kwa hamu

vile hunioni kwenye
makundi ya baa/
na bahati nzuri haujawahi
kusikia nikizushiwa uzushi
kitaa/ nakununulia
rubi kadhaa/ unahisi nakujali
k-mbe unampigia mbuzi gitaa

sometimes unanisongea nguna/
au wali ukidhani mi’ najali ilihali
sina habari, sina hisia siwazi
hata kukuonea huruma/
na sibadili dhambi hata
mbingu ikisogea nyuma

ah!
nashiriki nawe nyakati
twitter mpaka instagram/
picha unani-hashtag drunk in love/
nanunua brand za gharama za
hand bag/ perfume kali
simu ya ghali breakfast
zanzibar/

haimaanishi kuwa
tunaianza safari/
nataka nikuandalie maumivu
makali/ nahitaji nikuguse
ili kila unachokiona
kiwe kinafanya unik-mbuke
ni hatari

inaitwa zuia nanga kabla
bado haijang’oa/
maana haujaheshimu
mvua kama bado hujaloa/
kwa huu mchango ninaotoa/
ndo’ unafanya unazama
zaidi kiasi unaiwaza mipango
ya ndoa

jicho la tatu hauna
fungua jicho lako la pili/
utagundua kila ninachofanya
kwako batili/ unanipenda mno
ndo’ maana haujaona bado
dalili/ kuwa we sio wa kwanza
wala haupo kwenye
mpango wa pili
ah!!

unaniletea zawadi toka
majuu/ kuna wenzio
nilishawaacha
na walinichora tattoo/
mi sio tunda mama…
mama mi’ kidonda
utachelewa kusonga
ka’ bado unaingoja nafuu

sherehe ya birthday yako
kwenye ‘temple’ ya anasa/
umekuwa ’mental’ kwa
huu mwendo ndo’
umenasa/
kiasi unahisi huu ni upendo
na sasa/ hautambui kuwa
tukishiriki tendo tu nakuacha

kichwa changu hichi,kichwa
changu kishajadili/ kwamba
nitalala na wewe na
wewe na haifiki jumapili/
nitakuwa nimeshakuacha
ah! utanitafuta
kwenye simu ambayo
namba nitakuwa nishaibadili

utanitafuta mara mbili/
mara tatu kisha nne
utagundua kurudi
sina dalili/ ngoja ngoja
itang’ata moyo wako
kikatili/ mja wa
watu maumivu
hukujiandaa kuyakabili

utanipamba majina ya
kikafili/ sitasikia maana
nitakuwa mbali nishasafiri/
nishasahau utatunga nahau
kukanda mwili/ na huo
wakati haukuwahi kuutabiri/
ila upo

utaumia utashindwa kusimulia/
utaniulizia kwa wanaonijua
watakwambia/ kwamba
hauna tena chako
okota vipande vya moyo wako
nenda zako kaandike
tanzia

kisha watajua wenzio/
wanafiki watacheka
wanaokujali wataangua kilio/
watakusindikiza kulia/
watakupa pole wengine watasema
tulikuambia/ kuwa
wanaume wote mbwa!!

taswira itazongwa
na wingu/
picha utazichoma
kwa kisu/
utanitukana mara mwana
haramu mara malaya/
rafiki zako wakuu watakuwa
filamu na riwaya

wimbo niliokuimbia
kamwe hautokukonga/
utachoma mkuki moyoni
kisha kunyonga/
utaendelea kungoja/
utagundua mvumilivu
hali mbivu hiyo
methali iliongopa/
utagundua ilikuwa
ni soga/

hii itafanya ukonde
na kuanza/
kutumia pombe na ganja/
nayajua haya yote
kwa maana ndo nilikotoka/
utasimama kijasiri
na mwisho utadondoka/
‘sikiliza’

wataleta daktari
akuulize nini shida/
hawatapata
jawabu kabisa/
wataleta sheikh
wataleta mchungaji
wa kanisa/
watasahau kwamba
moyo uliovunjika
hauna tiba

natamani nikuambie kuwa nimekuteka makusudi/ maana unasikia na hujifunzi/ nikuumize kama mke w-ngu mpuuzi/ aliyekimbia na rafiki yangu siku moja baada ya harusi

nilishaambiwa na
mama nikapuuzia/
kuwa haujawahi
kupenda kama
haujawahi kulia/
kuna muda mtu mbaya
hutengwa na hatia/
maana kafiri hazaliwi
utengenezwa na dunia

ukijiua sitakuona
mzembe amini/
nitakuvalisha pete
ruksa uipeleke baharini/
najua tiba ya
upweke amini/
mwisho wako ni
kuwa kicheche kama
mimi

hapo utajua kunihuk-mu
sio haki/
mwanamke kama
wewe ndio amenifanya
niwe muasi/
bila hofu wala
kiwewe/
nitaendelea kuzunguka
kutafuta wasichana
vipofu kama wewe

sina hatia ..


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...