lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu dizasta vina – almasi

Loading...

nilikutana mtaani na mzee mmoja
tukaketi chini akanipa soga
mimi sitamsahau

alisema w~ngapi walikuwepo namba moja
sasa wamerudi chini ni vioja
watu wamewasahau

utavamia kwenye tamasha la muziki
usoni bashasha huku rohoni umeik~mbata dhiki
sanaa imesanda na sasa tena hauna kiki
utaigiza furaha kwa kunywa bia za mashabiki

zitaongea nguo ulizoazima kwa msela
hazitatosha kuficha ukweli kwamba hauna hela
hautak~mbukwa kama mwanzo wakati unatisha
paparazi hawatakujua so hautapigwa hata picha

hakuna atakayekuangalia usoni
tamasha utaingia kwa kuzidandia kuponi
mchumba uliyemmwaga atang’ang’aniwa kiunoni
utatabasamu huku hasira umeifungia moyoni

utapotaka kujichanganya utahisi haya
lipsi denda zitachakaa kusizi kaya
watasikika wadadisi wakiongea kwa kudisi
kamera zote zitamfata msanii uliyemu~inspire
hayatakuwepo majumba magari na mapochi nene
milo ya hoteli za kifahari na ma~roast kede
zitasahaulika idadi ya tuzo ulizohodhi kwenye majukwaa
huku magazeti yakiku~post mbele

hautatembeza tena rungu ka’ kipepe
hautavutia wachuchu maana nyota haina nguvu
hautafatwa tena na mashushushu kwa maseke
utak~mbuka ulivyozungukwa na grupu la vicheche

michuzi itakauka utapiga hodi ukame
hautawekwa kwenye ma~board ka’ van dame
hautashawishi magari road yapangane
na utakuwa peke yako bila ya ma~bodyguard nane

kipindi ambacho taswira yako ipo gado
ndo’ kipindi cha kulikata shauri lako
kutambua nafasi na thamani ya sauti yako
kutambua dhamana mapema kabla ya mauti yako

dhamana yako ni zaidi ya kula na kupiga pamba kali
kununua bupa na chupa ukizilaza chali
jina kubwa likikufumba ushindwe tafakari
utakufa masikini ukizubaa kuzichanga mali

usijesahau maisha yako halisi
yanayolingana na kipato chako thabiti
usijekufa kipindi ambacho michango haikidhi
haitoshi hata kujenga nyumba ya mama’ako kibiti
uko wakati wa k~miliki idhini ya uwongo wako
wenzako wamedondoka, je utajifunza?
unasifika mjini kwa wingi wa longo zako
ukifa tutasimulia nini watoto wako

tutasimulia idadi totoz ulizonusa
au gambe idadi ya kopo ulizoruka
idadi ya mahusiano au idadi ya mioyo uliyoivunja
au idadi ya wasichana wadogo uliowavuruga

najua mwisho mwanangu hamna njia
utatokewa na kila hadithi uliyoisikia
sicho kitu ninachokihofia
hofu yangu kama umeshaiandaa saikolojia

ukija wakati pazia halifunguki
wadananda uliowadandia hawakuk~mbuki
najua itafanya akili ichoke utapagawa
tafadhali usijegeukia pombe na madawa

kipandacho hushuka ulishawaza
si muiujiza ni asili inayoshangaza
wasahaulifu walimwengu ilitangazwa
watataja mashujaa na jina lako halitatajwa

wanafki, walafi na mabishoo zako
w~ngapi watakuwepo kiu ikidaka koo lako
muda wa kuwasoma wote waliopo kando yako
maana hata pesa haitatibu jelaha la roho yako
maagano ya siri yatakuwinda
vyote walivyotabiri vitafika
maisha ya ndoto yataisha
utairudia kawaida utagundua kuwa haukuwa malaika

kiasi utajua dini
utajua harufu ya sakafu kwa maana utakuwa chini
hata maana ya maisha itapotea
sumu, kisu na vitanzi vitasogea

sikutishi ila utakufa peke yako
jeneza lako halitabebwa na hao vicheche wako
sishangai wenge lako, ng’ombe
nashangaa unapoyumba kwa kuzidiwa na ukubwa wa pembe lako

ni heri kuwa mwewe
maana mwoga anajali kuwa uelewe
kundi la watoto nyumba wanakupenda
na wanaota siku moja waje kuwa kama wewe


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...