lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu dizasta vina – a father figure (official album intro)

Loading...

natazamwa kama mgongo
wa kuegewa kama chombo
nikitegemewa na watoto
lakini kwa ndani mi’ ni mtoto pia

mtoto wa katikati
njiapanda kati ya
ukweli na uongo
ukubwa na udogo ama
upofu na uchongo
ama pumbazo na mwongozo

katikati ya uhalisia
na mategemeo
karibu na jitihada
mbali na egemeo
sina hesabu ya mafanikio
kila kitu ni juk~mu na uwepo w~ngu
ndio huk~mu yangu ya leo

sina cha thamani nilichorithi
ila nilichonacho ni k~mbuk~mbu ya simulizi
na picha nilizokuwa nazo
nilizopewa na wavuja jasho
wasakatonge wa mwanzo kwahiyo
nigawie masikio yako
macho yalinipa tishio lenye manufaa kw~ngu
maana nilishuhudia kufanikiwa na
kushindwa kwa mashujaa w~ngu
lakini shuhuda zilinifunza

zilinifunza kuhusu mashujaa
wa karibu na mbali
wenye nasibu za ghali
au watabibu wa kuponya hali
na nguvu ya kuf~kuza shali
za wadhalimu na waharibifu
wenye visu vikali

mashujaa walisisimua sana
lakini wapo kadhaa waliokufa
na hawakuacha alama
nilifunzwa kuhusu hawa

hawa mashujaa walipanda maua
wakilea vyema yakachipua
na wengine usingizi ulipowachukua
wadudu wala mizizi wakaf~kua

machache yaliyofanikiwa kukua
ndege waliyachukua
na mengine hayakuwa mahala pema
kwahiyo yalichomwa na jua na kuungua
oooh hujui walimwengu walisema nini
kuhusu hawa shujaa w~ngu walioshindwa
walisema kaharibuu
kwakuwa shujaa kwa walimwengu
ni yule anayeweza wakati akifanya
lakini sio anayeshindwa wakati akijaribu

kwa walimwеngu shujaa
ni yule mwenye nguvu
asiyеtoa chozi wakati wa uchungu
asiyekosa au anayeonekana mtukufu
kwa walimwengu ushujaa ni
kuweza na sio kuthubutu

kwahiyo wakati sherehe za mashujaa
wao zikipikwa kuchochea
hadithi za mashujaa w~ngu
zilizikwa na kupotea

kwakuwa mashujaa w~ngu
hawakuvaa suti zenye nakshi na kuita
hawakuwa na viatu vya kung’ara hivyo
hawakupendeza kwenye jarida

ni kama walipima ushupavu wa mashujaa
kwa kuangalia afya za maua
bila kujua afya za maua sio ubora
wa anayeyajua pekee
lakini kuna jua na mvua na ni
ubashiri wa kujua lini vinakuja
uhakika ni kesho, kesho yenye giza
na hakuna anayeitambua
shujaa w~ngu alileta mlo mmoja
kuhakikisha siku haipiti, na aliweka
tofali moja wakati wa kujenga msingi
alif~gia barabara alipambana na
uraibu kama kamali, ulevi na madawa
ila hadithi yake haikuvutia gazeti
sio sawa

ni vile nimeanza kuwa kama shujaa
w~ngu nimegundua kuwa sijamaliza kujua
ni kama nimeanza kulea wakati sik~maliza kukua

natamani kuwa shujaa mzuri
lakini nipo hapa kujifunza
na pa kuanzia sipajui

sipajui maana maelekezo ni mengi saa hii
mara jikaze wewe, baba halii
mara utapoteza nafasi, watu hawatanii
mara kwanini usifanye kama nanihii
ona watoto wake wamenanihii

bahari ya elimu ni pana kuushinda upeo
kulia matarajio, kushoto mategemeo
bado najifunza sipo mbali
ila sijui lini nitakuwa tayari

inaniwia kuweka kipimo
cha kujua kipimo kiundani
kupima usahihi wa wito
ninaposema hadharani
unawaandaaje watoto kwenda mitaani
kwa sababu kuliko kuwa mkata maua vitani
ni bora kuwa mwanajeshi kwenye bustani

nini maana ya kuwa baba
ikiwa bado najifunza
kutosherehekewa nikishinda
ila kusakamwa nikianguka
hata nikipendwa au nikichukiwa
ni sawa ila si vyema nikapuuzwa
labda ninachelewa ila ni vyema
nimejua kuwa baba hazaliwi
anaundwa


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...