lirik lagu songa - niite
[intro]
yeaah… duke tachez.. yeeah
[ubeti wa kwanza]
yeah, kwa uzima nafungua kinywa nach0m-a hii habari
naisoma kwa kina vina vinatoboa ka’ bikari
nimepima homa kwenye roho ya hii sayari
wanasema n’na ngoma eti nakohoa mistari
sihitaji support kupost stanza nia
verse ni lugha mbili ka’ noti ya tanzania
vibaraka wana njaa, bosi anawaza mia
ni mkosi balaa, kitaa tozi anatanga njia
mbwiga hasifiki kwa ubingwa wa busara
ukiona giza na jogoo haliwiki ujue mida ya kulala
mc vipi? mbona huwakilishi shida ya f-kara?
au umeshapata tija umesahau tiba uchwara?
mdomo… hauachi tathmini ya amani ya mswaki
mtoa roho angepokea rushwa maskini gani angebaki?
stuck kwenye move mi’ ni mkali kwenye flow
na-scratch maujuzi m’ ni chaki we ni black wall
mzungu anaiga kwenye shida ndugu mungu
narusha machungu zaidi ya miba ya nungunungu
nyoa dungu huu ni msiba mbwiga tubu
nimeshika rungu nyumbu anasinywa ka’ sungusungu!
[kiitikio x2]
niite songa!
kanuni ya harakati
wana haraka wapo kati nabuni sina tamati
niite songa!
thamani ya muwajibikaji
maisha darasa huru na mi’ ndo muelimikaji
[ubeti wa pili]
wazazi wanasema nimeshakua
ina maana… vibaya na vyema nimeshajua
jua linazama tazama inanyesha mvua
nakesha kwa dua k-muombea anayekesha akivua
alfajiri inafika na mwezi unazama
jogoo la mbishi lawika na wezi wanahama
yamaanisha zienzi tenzi kwa ujenzi salama
uweze chutama j-po kuna washenzi wanabana
wanasema mi’ ni mkali ila why sisikiki?
bei ya sukari inafanya ninywe chai na pipi
rafiki… mnafiki hanifai kwa dhiki
n’nachomshukuru mungu tu uhai silipii
cheza pazuri, ukiweza eneza kauli
wajinga wanatoa macho ka’ wamepoteza nauli
tenzi shule kwa hizi tungo nik-mbuke
hizi verse nagawa bure kwenye midundo ya duke
[kiitikio x2]
[ubeti wa tatu]
baba ananiambia… maneno hayavunji kuti
sawa nachana ila mbona flow zangu hazifumi suti
mi’ mweusi roho yangu haifugi chuki
dada anasema usiposoma mdogo w-ngu utarudi bushi
meza ukweli kwa pressure uteme uongo
palla anasema mhaya nd’o kauleta umeme bongo
kama husajiliwi jitahidi uchenze ndondo
mwema mungu sio said anayesema ubebe gongo
sifuri ndio inaanza na moja ndio ya pili
cha ajabu ya pili inaanza na kwanza inasubiri
hoja ya kishamba haina haja ya kuijadili
hii ni hoja ya kijanja pata stanza na akili
hii mic ni shamba na mimi ndio mkulima
navuna ninachopanda na ulimi ndio unalima
hapa utaganda huu sio umwinyi na ujima
mzazi mwambie mwana mjini si pa kupima…
[kiitikio x2]
Lirik lagu lainnya:
- lirik lagu lil menace - low pro diss 1
- lirik lagu tramteatret - morgengry
- lirik lagu vys - run it up
- lirik lagu ty benjamin - one luv
- lirik lagu pj morton - winter wonderland
- lirik lagu dutch massive - dr. ama
- lirik lagu kazzy chase - go flow
- lirik lagu ill bill - canarsie high
- lirik lagu serena ryder - blue christmas
- lirik lagu luis coronel - hermano mio