lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu slimsal - target

Loading...

intro
watakwambia anga ni kikomo angalia juu … eh
waulize mbona mwezini kuna alama za miguu … whoa!
wao wanakutaka wewe kwao ndio target … yea mh!
nachotaka mimi nikuoneshe wewe target… woo!

verse 1
waafrika wanawatolea macho waamerika
waamerika wanawatoa macho waafrika
wenye nacho na wasonacho sayansi ya matabaka
waulize wenye nacho ni wapi walikipata
usiulize waso nacho ni w-ngapi wanakitaka
sema kipo wapi uone ni w-ngapi watakifata
upo sokoni kama msomi wa chuo kikuu
kwenda kujiuza kwenye interview
na hii picha view, ka ni picture of you
jua una fikra few mwambie boss fu
haijalishi hata kama hujawahi kwenda school
ama ulikwenda na ukaambulia ff tu
wakikwambia njoo tukemee madawa ya kulevya
waambie tumtafute yule anayeyatengeneza
huwenda tukaweza kuelewana kingereza
kwa maana si hatumjui nani anayeyapenyeza

chorus
watakwambia anga ni kikomo angalia juu yeaa… (juu juu juu juu yeaa)
waulize mbona mwezini kuna alama za miguu yeaa… (guu guu guu guu yeaa)
wao wanakutaka wewe kwao ndio target‚ nnachotaka mimi nikuoneshe wewe target
wao wanakutaka wewe kwao ndio target‚ nnachotaka mimi nikuoneshe wewe target

verse 2
wakionesha alama peace‚ hakuna aliye salama
sababu ni alama ya pistol, vidole vikikutana… yea!
kule ulipokimbia ndipo ukweli ulipofichwa mh!
maisha ya mtaani ni degree kibao ulimwengu ticha mh!
mlango wa sita wa fahamu ndio ufunguo wa maisha
zero mpya zipo instagram facebook twitter
mtandao ndo mtindio wa ubongo usiojificha
mtandao ndio mtandio wa uongo unaouficha
na siku moja, nitarudi kule tulipotoka
nikawaeleze washkaji zangu kuwa tulipotoka
na ndoto za kujenga maghorofa kwenye vichwa vya watoto wa kota yea!
ndoto za kuwa mwanamuziki nyota bongo movie na kucheza soka je?
wapi zile ndoto za kusoma kuja kuwa lawyer ama kuwa doctor… whoa!
uuh! shule haikunipa nilichokosa‚ mitihani haikunipima ilini-torture
walimu walinifunza kuwa mwoga, kwasababu niliwaogopa

chorus
watakwambia anga ni kikomo angalia juu yeaa… (juu juu juu juu yeaa)
waulize mbona mwezini kuna alama za miguu yeaa… (guu guu guu guu yeaa)
wao wanakutaka wewe kwao ndio target, nnachotaka mimi nikuoneshe wewe target
wao wanakutaka wewe kwao ndio target‚ nnachotaka mimi nikuoneshe wewe target


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...