lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu rapcha - dhahabu

Loading...

[intro: damian soul & rapcha]

takataka

takata

takataka

takata

takataka (what is dead may never die.. what is dead may ne..?)

imetakata

takataka

imekua dhahabu yang’aa

[verse 1: rapcha]

mshua kutumia tu kondomu yeye alikataa

alivyopewa story kuna mimba yangu alikataa

ikabidi mama ndo anipambae j~po mwanzo alipoulizwa home ka’ anamimba ‘ye alikataa
siku zikamove mara miezi ikajikataa

shule walipojua kuwa ana mimba tu wakamkataa

mwisho wa siku mama ndo akajifungua

maana hakupokea ushauri wa kutoa mimba ye alikataa

ado ado kabla ya kutembea nikaanza kutambaa

mama hakutoa macho yake kw~ngu kila saa

akipata dili za chapaa aliomba ndugu zake waangalie mtoto ye atoke wote wakakataa

kwa sababu zisizonihusu, majirani kuruhusu ncheze na watoto wao tu walikataa

mvua zikanyesha zikakata nikakua

nikagundua kuwa mshua hakuzingua

[chorus]

ona takataka leo imetakata

takataka sasa imetakata
takataka

imetakata

takataka

imekua dhahabu yang’aa

[verse 2]

nikaenda shule mwalimu wa hesabu akanikataa

group discussion wale smart wananikataa

nkaanza kujifunza kutongoza sio shule wala mtaa kila binti nnaemtaka ananikataa

kuna ambao kuongea na mimi tu wakakataa

wеngine wakaongea ila kunipa namba wakakataa

wenginе walinipa kwenye kukutana wakakataa

wengine ndo baada ya kuonana wakanikataa

nkitafuta nafasi ya kushine watu wananikataa
nkiwa lowkey ninaboa wananikataa

vyeti nimetembeza ka’ kahawa maofisini

mpaka nguo zangu wamekariri bado wamenikataa

watu wananiambia kuwa kujiriajiri ndo inafaa

nikijiajiri naona kama watu wananikataa

jua linaibuka linazama juu natazama

haya maisha mungu tu pekee ndo hajanikataa

[chorus]

ona takataka leo imetakata

takataka sasa imetakata

takataka

imetakata

takataka

imekua dhahabu yang’aa

[verse 3]

kama hukuelewa ule mstari wa mwisho kwenye verse ya kwanza skia

acha niiweke very clear

mshua alizingua tu kwa kile alichofanya pale ambapo ile story ya mimba yangu ilimfikia

mama nae naona hakuwa proud kunibeba muda ule na ndo maana kwa wazazi alikana akaninificha

all my life all my life all my life

nitatoka jasho nipende sipendi all my life

posa hazina idadi nimetuma karibia niimalize dar

leo wazazi watakubali binti atakataa

ntapoenda kesho binti atakubali wazazi watakataa

kama wote watakubali dini zinakataa

nimeamua kujipenda mimi kwanza
kwa kufanya hivyo siumizwi na yeyote anaenikataa

dunia in~z~di kuzunguka natusua

nagundua nahitaji kusamehe walionikataa

[chorus]

ona takataka leo imetakata

takataka sasa imetakata

takataka

imetakata

takataka

imekua dhahabu yang’aa

[outro: damian soul & rapcha]

takata

takata

(what is dead may never die.. what is dead may ne..??)

imetakata

takataka imetakata

takataka

imekua dhahabu yang’aa


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...