lirik lagu peen lawyer - ni uchochezi ni mchochezi
verse 1
waliomteka roma bash-te anawajua
tafakari zao pumba kwa utabiri wa mfalme juha
eti kabla ya jumapili vunja kidole cha mwisho
utanzania ni somo kama uraia ni fundisho
roma alikuwa na hogo na ikulu akawaimbia
ule haukuwa mchongo ni madudu yalinyapia
ah kweli bahati manji ana moyo wa chuma
maana moyo wa nyama kwa hizi kesi si ungesimama?
unataka kwenda zimbabwe ili niwe free
njoo ujerumani nikupe place for free ( dom)
kama moni kabla hajaifuta ile post
ntakuhost big mouse mpaka ditekta atalost
wasanii wenu wameuzwa utawala umewanunua
wapinzani wanateswa mabavu yanawasumbua
kutekwa kuteswa polisi na vipigo
ule sio uzalendo muulize ney wa mitego
chorus
ukipinga na uko rwanda ujue ni uchochezi
uganda ni uchochezi burundi ni uchochezi
hata kama ni zimbabwe ujue ni mchochezi
bongo hii? ni mchochezi ? bungeni ni mchochezi –ridia chorus x 2–
verse 2
miswahada kandamizi inapita ni hatari
maovu yanafichwa kuiokoa serikali
hoji uitwe mchochezi upewe kesi ya jinai
wanaongoza kitemi na ukibisha we huna uhai
ujinga nao ni ushenzi sawa na mmfuu hai
demokras ni andazi haki ndio yake chai
sio mbaya kukosea si wote ni binadamu
dhambi kurudia makosa ukiwa akili timamu
wanauliza nimetumwa najibu labda na mungu
sheria zikitoboka lissu anziba hizo tundu
nnshajitoa muhanga kutetea uonevu
j-po sheria ni mw-nga isiyohakisi mabavu
leo mi ndio naongea kabla kesho sij-potea
au yaje kunitokea kama yale ya kubenea
mwanadamu anaponikacha mungu ananisogelea
popote ye anafika iwe keko au segerea
chorus
ukipinga na uko rwanda ujue ni uchochezi
uganda ni uchochezi burundi ni uchochezi
hata kama ni zimbabwe ujue ni mchochezi
bongo hii? ni mchochezi ? bungeni ni mchochezi –ridia chorus x 2–
verse 3
anaejitia ukiziwi na upofu wa vyeti feki
tunajua mboga yake bash-te anaipiga jeki
hii laana ifike tis kuzimu mikocheni
moja kwa moja iende kudhulu magogoni
ikulu mdudu mchafu aliwe na python
salam kwa ofisa mchochezi nnayewindwa
siku ukipata chance nizime bullet ya ya kichwa
wahisani hawakati misaada kwao drama tunavyoteswa
hawajali huku mitaani kwamba saa nane alitekwa
lini ntaona haki na uzalendo wa hili bunge
jana aliyeitwa mwizi ndio leo anaendesha bunge
hata kijani ya jana kingunge ndio huyu leo
nasubiria machweo mawio bado kimeo
ukoloni uliacha mimba na utumwa umezaa leo
i am sorry mzawa africa viongozi wanafuga kero
katiba hazibadilishwi na nyingi zinakasoro
Lirik lagu lainnya:
- lirik lagu lave - washed wine
- lirik lagu ottoman turks - can't promise nothin'
- lirik lagu bonnie guitar - let him go
- lirik lagu cameronazi - slityawrist
- lirik lagu untel - gêne-ie-teur
- lirik lagu alory - decline
- lirik lagu soul demise - evidence of spoken words
- lirik lagu napoleon da legend - risks
- lirik lagu matt woods - stop
- lirik lagu airbag (banda argentina) - sonidos criminales