lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu one the incredible - kivyovyote

Loading...

verse 1:
huwa wanauliza na skiliza vipi, inapo skika beat
kwa hii mizani kwenye vina nashindwa ku-upima mziki
naposhika bic, watoto wanashika speech
mi dondoko, moko wa moto unamshika vipi?
chagua kujenga imani, au kujenga ghorofa
k-mtenga mpinzani au ku-mpa ushindani wakutosha
chagua kupenda ku ghani sio kutoka
yaani, uzeekee ndani ya fani usipewe promo ya kutosha
unapovunjwa moyo, unaujenga tena
na usiweke chuki, iache iondoke na iende vyema
usimtenge mpendwa kwa moyo, umpende tena
usipende kusema tenda apendacho na utende vyema
milele ntasimama nikidondosha fasihi
wanabana kwakua nimekataa kuipotosha jamii
ila mkali naheshimika ki-uhakika sio kwa zali
na habari ikifika wataiandika kila mahali

hook:
kwa hiyo wanangu msichoke
niko on play, o.n.e kwenye kipaza, nkikaza usiogope
bwana its o.k, mi naifanya all day
hata wakibana mi naifanya kivyovyote
kwa hiyo wanangu msichoke
niko on play, o.n.e kwenye kipaza, nkikaza usiogope
bwana its o.k, mi naifanya all day
hata wakibana mi naifanya kivyovyote

verse 2:
sasa nimekua kijana wa makamo na sifa
napanga vyangu kwa mtazamo na mifano ya uhakika
jambo afrika, nina jambo kwenye kichwa
kijana jenga msimamo kwani mahusiano huvunjika
moko sauti ya mtaa, uliza upate jibu
zaidi ya star, kivipi niende sawa na mawingu
mafanikio hafifu siyahitaji
kwani nlipo uanza mziki nlikuwa maskini mwenye kipaji
bado nipo town, chimbo underground mi napanga sound
bunduki kwenye mdundo utapagawa
wanataka niache ngumu nibane pua
ninyoe kiduku ndio niwe msanii wanaemtambua
ila, humu nilipo ndio unaponsikia
na kama haikushiki, hausiki, haitokusaidia
kule huku na njia
ila nacho sikia wasanii hawana stimu ka chupa tupu ya bia

hook:
kwa hiyo wanangu msichoke
niko on play, o.n.e kwenye kipaza, nkikaza usiogope
bwana its o.k, mi naifanya all day
hata wakibana mi naifanya kivyovyote
kwa hiyo wanangu msichoke
niko on play, o.n.e kwenye kipaza, nkikaza usiogope
bwana its o.k, mi naifanya all day
hata wakibana mi naifanya kivyovyote

verse 3:
w-ngependa wanifunge niwe mfungwa, nidundwe kama punda
ama sugu, niwe bubu wanidhulumu mpaka lugha
ila bado sumu, uliza kisumu mpaka arachuga
navuna kigumu kwani hakuna mgumu wakuzivuna
nyingi pole kwa wazazi, habari shilole
ni majanga, waganga wanafiki ka walokole
wapole w-ngapi watanipa pole wakati
mi sina stori na wanafiki nawapa dole la kati
nich0r- wakati sina, nipore wakati nina
siwezi kuwa mpole kwa hawa wakore wanaoninyima
wanauliza vipi saa ngapi, kivipi wakati
hii ni hivi, wakuifanya hivi wako wapi?
skiiza, huu ni umahiri sio dharau
kwa huu ushairi utak-mbuka usisahau
nipo town, nikimwaga sound kama spika
mshika dau, mi ndio dau lenye uhakika

hook:
kwa hiyo wanangu msichoke
niko on play, o.n.e kwenye kipaza, nkikaza usiogope
bwana its o.k, mi naifanya all day
hata wakibana mi naifanya kivyovyote
kwa hiyo wanangu msichoke
niko on play, o.n.e kwenye kipaza, nkikaza usiogope
bwana its o.k, mi naifanya all day
hata wakibana mi naifanya kivyovyote


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...