lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu ochuka - al inkishafi

Loading...

nilinde ulimi nisijehifadhi malipo ya dhambi
baada ya mwili kukosa hadhi kubadilikiwa rangi
bahari giza ya kutojua vipi itakuwa njiani
fahari beti, natulia tu ndio hisia zisiende duni
inasikitisha silaha kali
wanaumizana juu ya mauzo na fame kwenye kiwanda
kawaida ya ramani, roho imependa huwa haina kificho
moyo haujawahi kuuma
imani ninazokosa nazipata nikijitunza
ukitoa ulinzi vile dunia sometimes hutafsiri
mwisho maisha sio kifo
mara ngapi nimezikwa hali bovu bila mchongo?
so naomba ukae nami tutazame nyota angani
peponi rangi machozi beauty yako mbooni
wakati uhai unapokelewa mikononi mwa anayechonga hatma na hiari
sifuati muda kama vumbi ikinikuna moto za ndimi
mlemavu kiraka uzi
umetafuna vidonda kwa hivyo kupona siamini
tunahema kwa mic tujue ka we still breathing
penye kinyesi kuna ukombozi ingawa wengi tunakejeli
ndoa safi
ahsante ma ulinifunza itikadi mema
shukrani kwa ninayempenda kwa dhati
pete kidole nafinya piano
babu skiza nafsi yangu portal keys
pasipo mwanya ntamwaga wino
sadaka za imani
nitakufuata, hadi kwa giza ndani
kesho zikakuwa siku moja bila wewe
mlotangulia tukiwa msongamano zamani
nitakufuata hadi kwa giza ndani
nyumbani ikiwa tu pain
nichune denda nikumbatie, usniwache nidie lonely

hook:
ah ah
al inkishafi
tonesha donda wino safi

ah ah
al inkishafi
dunia, nyota mblamwezi

ah ah
al inkishafi
ndio nikiondoka fadhili yangu nafsi

naongoza beat hata dhidi ya maradhi moyoni
kisiwa cha maji machungu
hakuna raha
kifo baado hakina huruma
nachoma magode ndio nifukie kitabu cha mistari na moshi
mifupa kisu kufuma
kinara bonde za mauti
ajali ikawacha mtazamo na picha imechomeka
ka mjane na kasumba tamaduni
daftari ikitia alama mtihani zilikoseka
wanaoniinua nikiwa chini
rafiki sijawahitaja japo nikikumbuka machozi hunidondoka machoni
tarumbeta kwa wenye roho safi
pembeni sina hadhi
ila hakuna siku upendo wangu kwako umekuwa na tamati
nikiongezwa siku kwa kalendar
siku moja nitawatunza maua bikra tena tender
niko booth beti za weather
miale nishati n-n-surika kwa rehema
niondoke daraja pambio, zungusha santuri
fulusi haiwezikuinunua faraja
hakuna siku sina mtazamo wa jamii yangu huwaga
barua ya vita
ka monk -n-lemaza body natalaamika
bila courage sijui ka tungewahiheshimika
nikiwa broken, mziki hunifarijisha
msalaba ilizidi kisaliti
mwili ulichinjwa surgery
na mingi scars kwenye diary
takasa binadam kwenye sayari
kwa misa nimeghubika ubani
sometimes sorrow jangwani
ninapotazama miiba zimetoboa miili
upendo umelea nyuma jukwaani hawatakikufikiri
dini yangu elimu ya roho
sidhaminiki kidini ndo maana naitwa kafiri
underground africa
tumenajisiwa kwa nyeti hatujafarijika
pasipo kifo hakuna maisha tena
maandiko tuna kesha usiku kucha
klichoenda kirudi tena
chuma almasi matope johari
vita medali baada ya mbio kuishia kwa pri
kinembe keketa
makucha footprints zikifuatana kwa coma
jua liki-tupwa kaburi la jioni
ujana bila hata imani
wanauliza naandika vipi sheria za mlumbi
juu ya mlima nikaanguka ka malaika bila glory nikitema tembe kumi
ah ochuka
ka singekuwa infinity na nukta
ningekuwa muumba ala hisia zangu hulka


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...