lirik lagu music in me - maua ya jeneza
yamedhibitisha macho ninayosikia majirani wakinong’oneza
huna kidhibiti mwendo uko salama bila mkanda wa usalama
kama nyuki wakufuata buyu la asali wakuchovya wakulamba
umewatega
umewapendeza
unapendeza kama maua ya jeneza
aah kama maua ya jeneza
verse 1
vipodozi ngozi nyororo
ya kuwafunga macho
mavazi yasoficha uchi
manukato ya kuficha njia za mkato
tabasamu la kusisimua hamu
tunda la edeni tamu
haramu
hadithi ya kalamu yenye wino wa damu
chorus
yamedhibitisha macho ninayosikia majirani wakinong’oneza
huna kidhibiti mwendo uko salama bila mkanda wa usalama
kama nyuki wakufuata buyu la asali wakuchovya wakulamba
umewatega
umewapendeza
unapendeza kama maua ya jeneza
aah kama maua ya jeneza
verse 2
titi la mama ukaliaga juzi tu
na unawaita big daddy
kitandani unateleza kama nyoka pangoni
taka kata kiu mtoni
starehe itakugharimu njoo na kitu mf~koni
subiri
onja yake shubiri
kama raha yaua sumu ya nini
subiri
onja yake shubiri
kama raha yaua sumu ya nini
chorus
yamedhibitisha macho ninayosikia majirani wakinong’oneza
huna kidhibiti mwendo uko salama bila mkanda wa usalama
kama nyuki wakufuata buyu la asali wakuchovya wakulamba
umewatega
umеwapendeza
unapendеza kama maua ya jeneza
aah kama maua ya jeneza
verse 3
ujana ni moshi urembo ni moto na wanaume ni kuni
chakula jikoni
mlo kuiva slowly polepole
maisha mpishi
kwa hali tatanishi
karamu ya mchwa simanzi fiche
ooh simanzi fiche
na sahani kaburi
outro
yamedhibitisha macho
huna kidhibiti mwendo
kama nyuki wakufuata
umewatega
unapendeza kama maua ya jeneza
aah
Lirik lagu lainnya:
- lirik lagu kbrum - desce e sobe
- lirik lagu fedorets - sauce
- lirik lagu heather edgley - i don't need you
- lirik lagu sketti
- lirik lagu kurt donavon - don't let me go
- lirik lagu snowy white - i wish i could
- lirik lagu dakiid - trust issues (unmastered)
- lirik lagu peter maffay - river
- lirik lagu galo frito - mãe vs. filho
- lirik lagu brandon thakidd - broken bond