lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu dizasta vina - theluji

Loading...

anachota kwa vidole viwili
anachemsha kwa kijiko inanawili
inakuwa nyevu, anachukua bomba la sindano anaivuta
inajaa kisha anadunga mwili

akili inahama anaita stimu
radha tofauti, sawa na sukari na ndimu
kila stimu ikiisha anajiongezea
anazoea mwili unanasa anaanza kubobea

anajaribu kuacha anairudia
mwili unamlilia uraibu unamvizia
hataki uhalisia maana haujamvutia
anajianzishia uhalisi bandia
anasema

mwili unapoa akili inatosha tufani
kihali gani chombo akidondoka rubani
alitaka furaha, furaha imegota tutani
dawa inampa amani, amani aliyokosa nyumbani

anapoteza sura ya kisomo
anapoteza kazi, hamu ya chakula na ngono
raha anayoipata inakuwa siri yake
kiasi anauza mali kukidhi haja za mwili wake
muuzaji anaendelea kuuza
serikali inaendelea kuzuga
jamii inaendelea kuvunga
washikaji wanaendelea kuvuta
mtaa unaendelea kufa

usimuuzie madawa mwanangu
najua hii kazi inakupa mafao
tafakari yatamkuta mwanao
usimuuzie madawa mwanangu

starehe yake mpya inamvunja pochi
inamaliza afya lakini inamfuta chozi
inamweka mahala pasipoguswa na mwokozi
bahati mbaya damu inawasha anakuna ngozi

theluji inamfikisha mbinguni vyema
anaihusudu hali
kiasi anashuka anaiba mpaka mali ili arudi tena
anaisujudu ganzi

alikuwa na mchumba
walishare all the nice things you know?
dinner dates ice creams
walienda kwenye bata za mjini, k~mbi za movie
kuangalia sijui the black panthers sijui the vikings
leo yupo ila hatamaniki
haangaliki
bora angekuwa malaya au mlevi wa bapa nyingi
ningeelewa, leo ngada zinamfanya anakata ringi

wanasiasa wanabishana
mchungaji ibadani na polisi ofisini
wafanyabiashara wana idhini
na mtaani madawa
yanaendelea kuwalaza chini vijana

najua biashara inakupa mafao
kiasi kwamba unawaza jinsi kutupa mbachao
lakini usimuuzie ngada mwanangu
labda kesho yatamkuta mwanao, just think about it

labda hauna elimu sana
naomba tuongee ka’ wazazi maana
nimeuchoka huu ubazazi
unaofanya nahisi umepitwa na wakati
na unajua nakuheshimu mwana

sina nguvu ningekupeleka mahakamani, ila
uchumi wetu haufanani
mpambanaji leo nashindwa vitani
namzika mwanangu ‘asa mi’ nitazikwa na nani?
swali, una nguvu? ndio
haufanyi chochote kutafuta suluhu? sio
hauko mahabusu, familia yako tukufu
kwa hiyo unahisi haya mambo hayakuhusu, au sio?

usimuuzie madawa mwanangu

labda hii kazi inakupa mafao
tafakari yatamkuta mwanao
just think about it


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...