lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu dizasta vina - karibu duniani

Loading...

yeah
huh
nimekuleta duniani bila idhini
tega sikio kwa makini nikueleze
kabla hujabwaga manyanga chini
nataka uijue hii ngoma ndo’ uicheze
nikutoe utumwani
hata uchague dini yako mwenyewe
mimi baba yako kwahiyo naomba nielewe
hauwezi kupata mwingine , kamwe usiendeshwe na pembe zako
maisha yako yako mikononi mwako mwenyewe
naomba uijue hali yetu
umezaliwa na kuwa hapo ni safari ndefu
so, kipindi usiote ndefu usivimbe ufumbue macho
kisha uyatazame ya walimwengu ..tazame ya walimwengu
heshimu hili jina la ukoo
linda kama jinsi unavyoilinda hii roho
palipo uzalendo kuna moyo
na uzalendo unaanza na kuwa loyal
tabia ya upole ni shida kuisanifu
lakini amani na hekima ndo” majibu
hasira picha ya karibu inayokuziba usione mbali
kiasi uone tija kuinasibu
sitakuwepo kukupeleka kwenye toy store
ucheze nazo michezo kwenye korido
uwe mpuuzi ushindwe cheza na books
iwe nuksi kiasi uone revolution is not possible
siahidi kuwa baba mkamilifu
napambana j~po mi ganda la udhaifu
amani gharama usijingize kwenye bifu
kosea ujifunze ili usiigize utakatifu
kuna dini kama mia mwanangu
sijui ipi ni njia mwanangu
uifate ipi sina jibu
ningemfata mola nimuulize mbingu ingekuwa ikaribu
karibu duniani
karibu duniani
ah, karibu duniani
kua ujue tofauti ya halisi na batili kuhakiki na kubashiri
umasikini na utajiri usafiri
uone tofauti ya usafi na ukafiri
kisha ujiulize kama utaasi au utasawiri
tupa uongo mwanangu chukua tija
funga mdomo mwanangu fungua kichwa
punguza mwendo wengi walijifia kwa haraka
kwa sababu ya kukaidi sheria na mamlaka
ik~mbuke hii siku umekua baba
uliyasikia majuk~mu leo umeyajua sasa
mwanaume ulifichwa msosi tambua kwamba
hauwezi kuheshimu kazi kama hujajua shamba
kabla hujanishusha mi’ hadhi k~mbuka
nimekufunza nimekufuta kamasi
nimekuvisha kufuli nimeahirisha shughuli
utanizidi kiburi ila hauwezi ukaivuka tamati mwanangu
hamna urafiki na simba na mwanangu
hata akikufundisha kuwinda mwanangu
kuna siku atawinda kisha windo litamshinda
atakosa nyama na utahitaji k~mlinda mwanangu, usiue
mbivu mbichi ngumu rahisi na nyepesi
piga kitabu au uingie kijiji cha mapenzi
mwanangu ufuska utaua hadhi yako
nimekupa vyote ninavyovijua kazi kwako
ukweli kuhusu hivyo vyama vya siasa
chumba kimoja usijedanganywa na vitasa
zote game kama drafti drafti
usishangae kuziona kamati zenye kamati
pesa sabuni zitafute kila sku
ukipata usikate watu mwenye fedha ndo’ ana kisu
usisadiki kila tabasamu
kati yao kuna halisi kuna haramu
dadisi upate fahamu
karibu duniani
karibu duniani
asili haijali usawa tambua hilo
dunia ngumu kuzaliwa tu ni kuwa hero
hakikisha kisomo hakichezi mbali
so chunga ngono chunga mikono serikali
kisha uache kuvamia michakato
kama ambavyo ulikoma ziwa la mamaako
cha ndege kiota cha mtu sumu ukiishi nacho bila macho
mwanangu utazikwa siku si zako, heeh
usiwe mnyang’anyi tafuta fungu lako
ukidhurumiwa ujifunze kutokana na uchungu wako
maana utashushwa na utundu wako
poteza mali lakini usipoteze utu wako
pata shida umjue ndugu thabiti
k~mjua ndugu si rahisi
usidanganywe na uchungu wa dhiki
pesa ni nguvu lakini hekima ni nguvu zaidi, ah
ungali na afya jiongezee ujuzi
bahati ya jirani nayo usitembelee uchi
usiegemee kuti, kuwa na nidhamu
a’fu fadhiri binadamu ila usitegemee mchuzi
kua uone michongo inapofeli
mchungu muhogo muwa mmoko uliozamisha meli
propaganda na zogo na chokochoko
na utapewa uongo ili ujifunze kuiheshimu kweli
we mwafrika hauko simple una nguvu
ni vile uliibiwa history na mzungu
unachonena kinywani ni tija
kuna mstari mdogo kati ya amani na vita
penda kuwa na lugha nadhifu
maneno thabiti yanaunda uaminifu
acha masihara kaza mwendo ado ado
fanya ndoto kuwa malengo na malengo kuwa mpango
godd~mn i’m a father now, yeah
i can’t believe that i’m a father how?
nimeacha kushangaa shangaa so
nafanya kazi ukue, so you make your father proud
rafiki adhimu ni kazi
mweshimu kama unavyoheshimu wazazi
mweshimu jirani mbwa na binti yake
binti ni mlezi ukimuharibu jua umeharibu kizazi mwanangu
usijechoka kungojea
kamali ni mbaya usije omba kubobea
wajanja walipotea ogopa pombe na madawa
maana mwili mmoja hauna spare
karibu duniani
karibu duniani
karibu duniani


Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...