lirik.web.id
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

lirik lagu b boy blackfire - roho

Loading...

b boy blackfire from teamnguzo5 represent 255 (come on)

verse 1
natembea na hisia natembea na akili
nakutana na mengi ambayo nastahimili
ila bila ya roho hakuna faida ya mwili
inatunza yaliyowazi pia naficha ya siri

kua na roho ya subira ndio malengo yatimie
ukipata majonzi kaza roho usilie
ishi kwa amani kua na roho ya kirasi
roho ya upendo usiishi ukiwa na roho ya kinafki

ambayo haipendi kuona mapenzi ya dhati
mtu anaepoteza muda hawezi kupenda kazi!
usiwe na roho yenye choyo haitokidhi mahitaji
utaishia kufa maskini hata kama una kipaji

mungu ametuoa mwili ndani roho yenye hisia
haiwezi kuogea ila naamini inasikia
na ikipata huzuni mwili unakosa furaha pia
na ikishindwa kuhimili stress zinafatia

corus 1 (smart jr)
ubinafsi chuki manenooo hiyo ni roho ya namna gani?
mana ukarimu na upendooo hiyo ni roho ya kujalii.!
ubinafsi chuki manenooo hiyo ni roho ya namna gani?
mana ukarimu na upendooo hiyo ni roho ya kujalii.!

verse 2
wenye mafanikio wengi wana roho ya usikivu!
malaya ndio siku zote hua na roho yenye wivu!
kwa wapenzi wao ambao wana roho ya utulivu
roho yenye chuki kamwe haiwezi kuiona mbingu!

sipendi mzaha sina roho ya utani!
mama alishauri “niwe na roho ya imani”
roho ya siri inayoweza kutunza mambo ya ndani
sio roho ya kujisifia nikimpata malaya fulani

dada punguza roho ya kupenda
inakuponza kila siku matozi wanakutenda
ukiwa na roho ya huruma kila mtu atakutenda
kua na roho ya ujasiri fikiri kabla ya kutenda

sauti ya ghetto nina roho ya shetani
roho ambayo isiyopenda kushindwa kwenye medani
ukiwa na roho kama yangu utapingwa sana mtaani
na wasioweza kutofautisha kati ya picha na ramani

corus 2 (smart jr)
ubinafsi chuki manenooo hiyo ni roho ya namna gani?
mana ukarimu na upendooo hiyo ni roho ya kujalii.!
ubinafsi chuki manenooo hiyo ni roho ya namna gani?
mana ukarimu na upendooo hiyo ni roho ya kujalii.!

mama wa kambo kwanini una roho ya tamaa???
mfano wa chui asiyekua na roho ya kuzaa?
roho yenye giza haing’ai hata imulikwe kwa taa?
inabaki nyeusiii zaidi ya lami au mkaa???

nawasifu wenye roho ya ukatili!!
roho ya kibabe roho waliyopewa majangiri!
kutoa roho inahitajika roho ya ujasiri
sio roho kama yangu isiyoweza kustahimili

“roho inabeba siri za ubongo
sio mwanasiasa anabeba siri za uongo
bora jambazi anabeba siri za michongo
au maiti aliyebeba siri za udongo”

natambua bila roho siwezi kuishi
roho ya mjinga husema “bila mpenzi siwezi kuishi”
anasahau anaishi akiwa na roho thabiti
labda baba vinginevyo sina roho ya kurithi.!

corus 3 (smart jr)
ubinafsi chuki manenooo hiyo ni roho ya namna gani?
mana ukarimu na upendooo hiyo ni roho ya kujalii.!
ubinafsi chuki manenooo hiyo ni roho ya namna gani?
mana ukarimu na upendooo hiyo ni roho ya kujalii.!

Lirik lagu lainnya:

LIRIK YANG LAGI HITS MINGGU INI

Loading...